Millamboยฎ
Millamboยฎ

@Millambo_

16 Tweets 23 reads Feb 13, 2023
Kwanini Usinywe JUISI YA MATUNDA ya Kutengeneza Mtaani au Nyumbani ๐Ÿ˜Ž
Utakuwa umewahi kusikia, SUKARI ni adui namba 1 wa afya. Si ndio ๐Ÿ™…โ€โ™‚๏ธ
Sasa, nimekuelezea kwa lugha nyepesi kabisa. Kwanini juisi ya kutengeneza pia sio nzuri kwa afya yako.
๐Ÿงต๐Ÿ“ข
RETWEET Wajifunze wengi ๐Ÿ™
Kila ninapokumbusha watu wasinywe au kupunguza juisi za matunda, basi watu wanakuwa wakali kweli ๐Ÿ˜…
Sasa leo tujadili hapa.
Mwili wa mwanadamu umeumbwa kutambua viinilishe pale unapokunywa au kula kitu.
So, ukila au ukinywa mwili haujui hayo. Wenyewe unatambua viinilishe tu.
So, ukila stafeli utapata viinilishe (madini + vitamins), hata ukitengeneza juisi mwili utapata viinilishe vile vile, japo vitakuwa refined.
Tofauti ni kuwa kwenye stafeli utapata pia nyuzinyuzi (fiber). Kwenye juisi fiber zinaondolewa kama uchafu.
๐Ÿ“ŒSababu kubwa kwanini usinywe juisi, ni kuwa imetiwa maji mengi na kudilute viinilishe.
Na kuifanya kukosa ladha.
Kwa sababu maji mengi huongezwa kwenye juisi, inawalazimu watengenezaji kuongeza SUKARI ili kuifanya tamu.
๐Ÿ”—Wewe ukiuziwa juisi ya matunda iliyoongezwa maji mengi na haina sukari utakunywa? Jibu ni Hapna, haitakuwa na ladha/utamu.
Ndo maana sasa tunakataa juisi ya matunda. Imeongezwa sukari nyingi.
Hapa machawi ni sukari tu.
๐Ÿ“ŒKwa nini uepuke sukari?
Mwili wa mwanadamu unatengeneza nishati kutoka kwenye sukari na vyakula vya wanga + mafuta.
Binadamu anatumia sukari kidogo sana. Watu wengi wamezoea kula sukari nyingi + (wanga) bila kujua madhara yake.
๐Ÿ“ŒUnapokula, sukari kiduchu huzalisha nishati ndani ya mwili, inayobaki hugeuzwa kuwa mafuta na kuhifadhiwa ndani ya mwili. Hapo ndo kitambi kinapoota.
Sasa kama una kitambi maana yake umekula sukari nyingi sana ambayo kila siku inafanywa mafuta na kuhifadhiwa ndani ya mwili.
๐Ÿ”—Na ili kukitoa kitambi, ni lazima utumie mbinu ile ile.
Kuacha vyakula vya sukari+wanga ili kuulazimisha mwili uyeyushe mafuta kwa kutengeneza nishati kupitia mafuta yaliyohifadhiwa mwilini.
Hapo ndipo mwili utapungua.
๐Ÿ“ŒSasa,
Unashauriwa kula matunda yenyewe jinsi yalivyo au ukilazimika kusaga basi tengeneza smoothie.
Smoothie ni matunda yaliyosagwa yenyewe bila kuweka maji kabisa, au kuweka kidogo sana.
Unaweza kuchanganya na matunda kadhaa lakini bila kutia sukari.
๐Ÿ“ŒUnapokuwa umefikia hatua ya kushauriwa kutokula sukari. Mfano, wenye vitambi, kisukari, nguvu za kiume, magonjwa ya moyo n.k.
Hawa hulazimika kuacha sukari na vyakula vyote vya wanga vinavyoweza kupandisha sukari.
Ndo maana juisi ya matunda inakuwa ni hatari pia.
Kwa wagonjwa wa kisukari, au yeyote ambaye hatakiwi kupandisha sukari, ukinywa soda au juisi yenye sukari unapandisha sukari ya mwili ghafla, jambo ambalo ni sio jema. Kwa sababu ni kimiminika.
๐Ÿ–‹๏ธUkila embe au ndizi utapata sukari, lakini Mungu aliumba matunda kwa kuyaweka nyuzinyuzi (fiber) na viinelilshe vingine (vitamins+madini).
Ukila matunda, fiber zinakufanya ushibe haraka, lakini pia kudhibiti sukari kuingia ghafla mwilini na kupandisha sukari kwenye damu.
๐Ÿ”—Hivyo, kula matunda kunakufanya kupata sukari taratibu bila kuipandisha ghafla.
Ndo maana unashauriwa kutokunya juisi ya matunda ya kutengeneza nyumbani na mtaani.
Juisi za dukani ndio disaster kabisa.
Zinatiwa sukari za ajabu, zinaongezwa preservatives ili zikae bila kuharibika kwa muda mrefu.
๐Ÿ“ŒSasa,
Kula unavyoweza, kula unavyopenda.
Ukishauriwa kutokula sukari na vyakula vya wanga, hapa, juisi ya matunda nayo haitokufaa,
Ila kama hauna sababu ya kuacha kula sukari, wewe piga tu. Fresh.
Lkaini kitaalamu, sukari ya kuongeza kwenye vyakula si rafiki kiafya.
Ili kujifunza zaidi kwenye Bio Hacking na Personal development and branding:
FOLLOW ME: @millambo_
youtu.be
Chapa RETWEET Wengi wajifunze ๐Ÿ™

Loading suggestions...